21 Aprili 2025 - 23:00
Source: IQNA
Iran yafungua Maonyesho ya Kaligrafia ya Qur'ani Jeddah

Maonyesho ya Kaligrafia ya Qur'ani na Mashairi ya Kiarabu, yaliyoandaliwa na Ubalozi Mdogo wa Iran mjini Jeddah, yamefunguliwa rasmi katika mji huo wa bandari wa Saudi Arabia.

Tukio hilo lilizinduliwa na Farid bin Saad Al-Shahri, Mkurugenzi Mkuu wa tawi la Makka la Wizara ya Mambo ya Nje, kwa ushirikiano na Jumba la Makumbusho la Kituo cha Sanaa za Kiislamu cha Saudi Arabia.

Hafla ya ufunguzi ilihudhuriwa na Hassan Zarnegar, Mkuu wa Ubalozi mdogo wa Iran mjini Jeddah, pamoja na wanadiplomasia wengine, wawakilishi wa mashirika ya biashara, watu mashuhuri wa kitamaduni na kisanaa, na wajumbe kutoka mashirika ya kimataifa.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Zarnegar amesema jina la maonyesho hayo limechochewa na Surah Al-Qalam (“Kalamu”) kutoka katika Qur'ani, ambayo ina “alama za kina kuhusu kuandika na utafutaji wa maarifa.”

Amesisitiza nafasi ya sanaa katika kujenga madaraja ya kimataifa, alisema, “Sanaa na utamaduni ni miongoni mwa nyenzo zenye nguvu zaidi kwa ajili ya amani na ushirikiano.”

Aidha amesisitiza kuwa maonyesho ya kisanaa yanaweza kuwa majukwaa ya kukuza ujumbe wa “amani” kati ya mataifa.

Halikadhalika ametoa wito wa kuongezeka kwa uwekezaji katika ushirikiano wa kitamaduni, akisema kuwa hatua hiyo itaimarisha uhusiano wa kirafiki kati ya nchi. “Iran na Saudi Arabia ni nyumbani kwa ustaarabu wa kale na urithi wa kitamaduni ulio tajiri,” alisema, na kuongeza kuwa mataifa yote mawili yanashiriki dhamira ya pamoja ya kuhifadhi mila za Kiislamu na Qur’ani.

Zarnegar alihitimisha kwa kuwashukuru washiriki kwa kuhudhuria tukio hilo na akaeleza kuwa mipango kama hiyo inaonyesha nia ya pamoja ya “kuishi kwa pamoja kiutamaduni na kuimarisha uelewano wa kikanda.”

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha